Jumatatu, 14 Julai 2014

Wawili wahofiwa kupoteza maisha

WATU WAWILI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA BAADA KUFUNIKWA NA KIFUSI MKOANI KILIMANJARO by GLOBAL 13 minutes ago WATU zaidi ya wawili wanadhaniwa kupoteza maisha baada ya kufunikwa na kifusi wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji wa miamba kwa ajili ya uchongaji wa matofali. Tayari mpaka sasa mwili wa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Bless Adrian, mkazi wa kijiji cha Nganjoni wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro umepatikana. Juhudi za kutafuta miili mingine inaendelea licha ya kukabiliwa na changamoto ya zana za kufukulia kifusi.

Ujerumani ndo bingwa wa mwaka huu

Ujerumani wanakuwa timu ya kwanza ya kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika mchuano ulioandaliwa Kusini mwa Marekani. Ujerumani ilihitaji bao la muda wa ziada la Mario Gotze kuinyamazisha Argentina katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Maracana. Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia. Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa "Golden Glove". Japokuwa alishindwa kutwaa ubingwa wa dunia Lionel messi alitawazwa kuwa Mshindi wa tuzo ya "Golden Ball" akiwa ni mchezaji bora. Michuano ijayo ya kombe la dunia itaandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.