Jumatatu, 14 Julai 2014
Ujerumani ndo bingwa wa mwaka huu
Ujerumani wanakuwa timu ya kwanza ya kutoka bara Ulaya kutwaa kombe la dunia katika mchuano ulioandaliwa Kusini mwa Marekani.
Ujerumani ilihitaji bao la muda wa ziada la Mario Gotze kuinyamazisha Argentina katika mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Maracana.
Kufuatia ushindi huo Ujerumani walinyakua taji la nne la dunia.
Kipa wa Ujerumani Manuel Nuer alitawazwa kuwa kipa bora na akatuzwa "Golden Glove".
Japokuwa alishindwa kutwaa ubingwa wa dunia Lionel messi alitawazwa kuwa Mshindi wa tuzo ya "Golden Ball" akiwa ni mchezaji bora.
Michuano ijayo ya kombe la dunia itaandaliwa nchini Urusi mwaka wa 2018.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni