Alhamisi, 16 Februari 2017

Baada Ya Arsenal Kuchezea Kichapo Cha Bao 5-1 Kutoka kwa Buyern Munich

Bayern 5 vs Arsenal 1

Natamani kuamini kuwa sasa Wenger atakuwa anabet... Kwa mechi muhimu na yenye ushindani kama ya leo ana sababu gani za msingi za kutowaanzisha wachezaji wake tegemeo kama Giroud, Walcot na Chezk... Kulikuwa na sababu gani ya msingi ya kumtoa Konscienly dakika ya 60 na kumuingiza Gabriel?

Hatukatai Arsenal ina kikosi kidogo ila kwa matokeo ya leo imejitakia na Wenger amehusika sana kuibomoa..

Yaan kweli uongozi wa Arsenal umemuongezea mkataba wa miaka miwili huyu mzee.. Nafikiri kuna ndumba hapa.... Hivi kocha hajisikii aibu kwa matokeo mabovu daily!? Kiukweli inauma sana. Why Wenger unatufanyia hivi? Hivi hujisikii aibu na ukachukua hatua stahili za kuwajibika kama Meneja ukaamua kujiuzulu bila shuruti? Utaonekana shujaa sana. Kuliko kuja kufungashiwa virago vyako kama makocha wa timu nyingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni